Makamu
Mwenyekiti wa kundi la wabunge wa Tanzania wanaojihusisha na hifadhi
endelevu ya maliasili na matumizi endelevu ya mazingira (TPGSNRC),
Othman Mfutakamba akiangalia meno ya tembo wakati wa maadhimisho ya siku
ya tembo kitaifa iliyokuwa na kaulimbiu ‘Jiunge katika mapambano dhidi
ya ujangili wa tembo’ yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini
Dar es Salaam jana. Katikati ni Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli
na askari wa wanyamapori, Emmanuel Katambi.
Gari
la Maliasili likiwa limebeba Meno ya Tembo, wakati wa kujiandaa na
Maandamano kuelekea Mlimani city kwa ajili ya maadhimisho hayo
Msanii
wa Muziki wa Kitanzania Mrisho Mpoto akianza kuongoza maandamano kutoka
Chuo kikuu cha Dar es salaam Kuelekea Ukumbi wa Mlimani City leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...