Timu ya KMKM ya Kisiwani Pemba ikifurahia ushindi wake wa Ngao ya Jamii,mara baara ya kuifunga timu ya Chuoni mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika tisini ya mchezo kwa kufunguma bao 1-1.Mchezo huo ulipigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba ikiwa ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar.
Mgeni Rasmi katika Mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar na kuwaniwa kwa Ngao ya Jamii,Waziri wa Serikali ya Mapinduzi asiekuwa na Wizara Maalum,Mh. Haji Faki Shaali (wa pili kushoto) akikabidhi Ngao ya Jamii kwa Nahodha wa timu ya KMKM,Ame Hamis Kibobeo mara baada ya kutwaa Ngao hiyo kwa kufunga timu ya Chuoni kwa mikwaju ya penati 5-4,katika mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.
Kikosi cha Timu ya Chuoni FC
Kikosi cha Timu ya KMKM.
Beki wa Timu ya Chuoni akijaribu kutaka kuondosha hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake.
Mshambuliaji wa Timu ya KMKM,Juma Mbwana (8) akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Timu ya Chuoni,Mwinyi Haji wakati wa Mchezo wao wa kuwania Ngao ya Jamii,uliochezwa jana Usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.hadi mwisho wa mchezo timu ya KMKM ilishinda kwa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...