Na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 WAHAMIAJI haramu wapatao 18 wote raia wa Ethiopia,wamekamatwa mkoani Kilimanjaro wakiwa njiani kusafrishwa kwenda mikoa ya kusini na baadaye kuvuka mpaka wa Tanzania kwenda Afrika Kusini. 
 Wengi wa wahamiaji hao haramu ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 20 na 27 ambao wlikamatwa majira ya saa 6:30 usiku wa kuamkia leo wakiwa ndani ya gari lenye namba za usajaili T858AHW likiwa na tela lake lenye namba za usajili T419AAE mali ya kampuni ya SUNVIC ya Jijini Arusha. 
 Mkuu wa uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro Johanes Msumule amesema wahamiaji hao haramu walikamatwa katika eneo la Kichwa ng’ombe wilayani Mwanga kwa ushirikiano na maofisa wa uhamiaji na askari wa jeshi la polisi. 
 Alisema baada ya kukamatwa kwa gari hilo dereva alifanikiwa kuchomoa funguo wa gari na kisha kukimbia kusikojulikana na kuamua kilitelekeza gari hilo katika katika eneo la Kifaru na kwamba juhudi za kumtafuta dereva huyo zinaendelea. 
 Msumule alisema kutokana na kitendo hicho cha dereva kukimbia na funguo wa gari hilo,Maofisa wa uhamiaji walilazimika kuwasiliana na wamiliki wa gari ambao ni kampuni ya SUNVIC ndipo walipowapatia funguo nyingine. 
 “Baada ya dereva wa gari kukimbia na funguo tulishindwa kuliondoa katika eneo la tukio ndipo tukawasiliana na kampuni inayomiliki Lori hilo iliyoko jijini Arusha ambao walitupatia ushirikiano mkubwa ,hatimaye mchana walituletea funguzo za gari hilo.”alisema Msumule. 
 Msumule alitoa onyo kwa wahamiaji haramu pamoja na wale wanao wasaidia ikiwa ni pamoja na kuwasafirisha pamoja na kuwahifadhi kuwa idara yake imejipanga vyema kukomesha biashara hiyo. 
 “Kama nilivyozungumza hapo siku za mwanzo,tunataka biashara hii katika mkoa weru wa Kilimanjaro ifutike kabisa,hatuna utani na hatutaki mtu achezee shughuli hii tunayoenda kuifanya “alisema Msumule.
 Wahamiaji haramu waliokamatwa wilayani Mwanga wakiwa katika gari lenye tela.baada ya kufikishwa makao makuu ya uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi. Picha zote na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HONGERA SANA UHAMIAJI KILIMANJARO.
    TUNAOMBA UHAMIAJI NA UONGOZI WA SERIKALI MKOANI ARUSHA WAFANYE KAZI WAHAMIAJI HARAUM WAPO WENGI SANA ARUSHA PENGINE KULIKO HATA HUKO NGARA NA KIGOMA TAFADHALINI SANA SERIKALI ARUSHA MSIBWETEKE.

    KWENYE NYUMBA ZA KUPANGA MAENEO MENGI YA SAKINA NA KATIKATI YA MJI WAPO WENGI TENA WENGINE UTASHANGAA CHUMBA KIMOJA WANAKA WATU HATA ZAIDI YA KUMI. MAGESA MULONGO NA WATU WAKO PLEASE MSILALE.

    ReplyDelete
  2. Wewe hapo juu hujasoma kuwa hawa wahamiaji walikuwa wakielekea afrika kusini?

    Mie mwenywewe nimefika south afrika na wabongo kibao wamijipa ukimbizi. Maisha yanasababisha watu wawe wahamiaji haramu na hivyo ujuwe hata wa TZ wengi wako nchi za watu kama wahamiaji haramu. Tuwaone huruma hawa watu , kwa ajili hamna mtu anatak aondoke kwao na kujazwa kwenye trela la lorry

    ReplyDelete
  3. Hawa wahamiaji haramu wameshaona udhaifu wa serikali . Wenye kazinzao hawafanyi mpaka rais aingilie kati

    ReplyDelete
  4. Jamani hao ni njaa kwa kwenda mbele.

    Muwahurumie.

    ReplyDelete
  5. Viongozi wote Africa wanaona jinsi gani vijana wanateseka kutoka makwao wakienda nchi zingine kwa maana ya kutafuta maisha,wajiulize maswali ni kwanini vijana wanafanya maamuzi kama hayo, na pia watafute njia ya kuwasaidia na sio wawe wakinyanyasika tu kwa kutanga tanga.Huko pia wanakokwenda sio salama iwe ulaya ama hapa Africa.Please viongozi wakikutana Adiis Ababa watafakari juu ya hilo,pamoja na usalama kwa ujumla wake.

    ReplyDelete
  6. Kwa hiyo! waachwe tuu wageuze Tanzania Shamba la Bibi kama wanavyofanya wawekezaji feki tutapona kweli? Kuweje na Nashangaa Watanzania wanao zamia ilhali wenzao wanakimbilia Tanzania nchi ya asali na maziwa. Mtanzania anaye zamia ni wale wasiopenda kuchapa kazi, na kutokea jasho mazao. Wakwepa umande.

    Haya fursa ya kujenga Katiba hiyoooo. tumewezesha vipi masuala yenye kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania ki kweli kweliii? tuache domo domo, tutende.

    ReplyDelete
  7. Mnhhh!!!

    Kweli Wadau wa Westgate-Nairobi hawakosekani kundini humo?

    Wanaweza wakamaliza kazi Nairobi na wakafunga safari kwenda Kusini kwa Madiba kupitia Tanzania!

    Mara zote penye Msafara wa Mamba Kenge hawakosekani!

    ReplyDelete
  8. Vijana wa Desalegn Hailemariam (Raisi wa Ethiopia) kwenu kuna nini?.

    Ni kweli vijana kwenye nchi zoe ni watukutu na hupenda safari hata sisi Tanzania vijana wetu wanasafiri lakini sio makundi kwa marundo kama ninyi Waethiopia , na mara zote Wabongo wakisafiri hurudi nyumbani!!!

    ReplyDelete
  9. Wapelekeni Zanzibar wakapewe vitambulisho vya ukaazi na vya kupigia Kura.

    ReplyDelete
  10. POLENI SANA NDUGU NA KARIBUNI LONDON BOX INALIPA SANA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...