Mwili wa Wakili Israel Magesa  (pichani) aliefariki dunia jana  asubuhi,unatarajiwa kuagagwa siku ya Jumamosi tarehe 07/09/2013 kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam,kuanzia Saa 5 asubuhi.

Mwili unatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili tarehe 08/09/2013 asubuhi,kuelekea kijijini kwao Chitare,Majita,Musoma kwa Mazishi.


Wakili Magesa, ambaye  alikuwa ni mmiliki wa kampuni ya Mawakili ya Magesa &Co. Advocates, ni baba  mzazi wa Phares Magesa (MNEC), Kalimba Magesa, Makongo Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na baba Mkwe wa Haika Lawere.

Wakili Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu, Msajili wa Mahakama kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International - Tanzania Chapter, pia ni mmoja wa wanasiasa waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini.


Enzi za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, na alikuwa ni miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.


Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na shughuli rasmi ya kuaga itafanyika ijumaa tarehe 6/9/2013 kuanzia Saa 5 asubuhi Dares Salaam na mazishi yatafanyika siku ya jumapili 8/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...