Naibu waziri wa maji na mbunge wa jimbo la makete Dkt Binilith Mahenge akitoa hotuba yake kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa chuo hicho Bw. Tekeleza Mahenge akisoma risala ya chuo.
Msaidizi wa askofu Philemon Kahuka akiongea kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wakifurahia.
Habari/picha na Edwin Moshi, Makete
Kutokana na kuwepo kwa baadhi ya watumishi katika sekta ya afya nchini kuwa na sifa mbaya, wito umetolewa kwa watumishi wapya wanaoingia katika ajira hiyo kuondokana na matatizo kama hayo kwa kuwa yanaepukika
Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na mbunge wa jimbo la Makete ambaye pia nia naibu waziri wa maji Dk. Binilith Mahenge wakati wa mahafali ya 6 ya chuo cha tabibu na uuguzi Bulongwa kilichopo wilaya ya Makete mkoani Njombe chini ya kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya kusini kati
Dk Mahenge amesema kumekuwepo na baadhi ya watumishi wa sekta ya afya ambao wamekuwa na sifa mbaya ikiwemo lugha mbaya ama kutoa dawa feki na zilizokwisha muda wa matumizi kwa mgonjwa jambo linaloitia doa tasnia hiyo hivyo kuwataka wahitimu hao kuwa mfano bora kwa jamii kwa kuondokana na kashfa kama hizo
"Tunaamini ninyi mmefunzwa vizuri na mna uchungu na taaluma yenu, tunawaomba mkawe bora na mchape kazi kwa moyo mmoja ili kuinua sifa ya chuo lakini pia kuwawekea mazingira mazuri hawa wanaokuja nyuma kwani mkifanya vizuri mtaajiriwa na hawa wanaokuja nyuma yenu mtawasafishia njia ya ajira kiurahisi" alisema Dk Mahenge
Awali akimkaribisha waziri Mahenge, msaidizi wa askofu wa dayosisi ya kusini kati Mchungaji Philemon Kahuka amesema wanajivunia kuzalisha wanafunzi wenye maadili mema na wanaofanya kazi kwa kujituma kwani wanapokea sifa nzuri kwa ambao wapo kwenye ajira na wamesoma katika chuo hicho cha Bulongwa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...