Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina,sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu,iliyofanyika leo,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa Gold Crest.
  Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kubweteka na kuisubiri Serikali iwaletee ama iwafanyia kila kitu hapo walipo.
 Sehemu ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya Max Malipo inavyoweza kuisaidia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Baadhi Washiriki wakifuatilia.
PICHA ZADI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mhe.Nawanda, Mhe.Massele na Mhe. Makamba tunashukuru kwa Mchango wenu juu ya Fursa zinzopatikana,

    Kwa pamoja twenzetu!!!

    ReplyDelete
  2. Swali:Kwa nini viongozi wetu hawatumii lugha ya taifa(Kiswahili)kuhutubu kwenye makongamano ya kimataifa ?Nahisi sababu kiingereza sio lugha yetu hivyo wenye lughe yao hupata taabu sana kutuelewa,mfano wa baraza la umoja wa mataifa -NY.
    Mh. Rais angetumia kiswahili ingekuwa vizuri sana kama wale wa nchi nyingine wanavyotumia lughe zao.
    Maana pia kwa kutumia lughe yako utaweza kueleza yale maoni yako kirahisi na kukabidhi hiyo hutuba kwa lugha ya kiingereza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...