Naibu Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Mh Januari Makamba akizungumza kwenye mada yake iliyohusu masuala mbalimbali, kuhusiana na Fursa ya kuongeza thamani na kutengeneza jina,sambamba na fursa ya matumizi ya Teknolojia mbele ya maelfu ya vijana waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzzetu,iliyofanyika leo,ndani ya ukumbi Gold Crest,jijini Mwanza.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akizungumza mada
iliyohusu fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nishati na madini ndani
ya semina ya kamata fursa twendzetu,iliyofanyika mapema leo ndani ya
ukumbi wa Gold Crest.
Naibu
Waziri wa Nishati na Madini,Mh Stephen Masele akimtambulisha mmiliki wa
hotel kubwa ya kitalii hapa jijini Mwanza, Gold Crest,Bwa.Mathias
Erasto,ambaye pia ni mchimbaji mdogo wa madini,aliyajipatia fursa
mbalimbali na kuzitumia ipasavyo na kufikia hapo alipo kimafanikio.
Mkuu
wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida,Mh.Yahaya Nawanda akizungumzia mada
yake iliyohusu suala la ufugaji,hasa kuku wilayani mwake,ambapo pia
amewataka vijana kuitumia fursa ya ufugaji wa aina yoyote katika suala
zima la kujiletea maendeleo kwa namna moja ama nyingine badala ya kubweteka na kuisubiri Serikali iwaletee ama iwafanyia kila kitu hapo walipo.
Sehemu ya wakazi wa mji wa Mwanza waliojitokeza kwa wingi mapema leo kwenye semina ya kamata fursa twendzetu,wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo,ambapo mada mbalimbali zilikuwa zikizungumzwa.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Maxcom inayouza bidhaa yake ijulikanayo kama Max
Malipo,Bwa.Juma Rajab akizungumzia kuhusiana na fursa ya bidhaa yake ya
Max Malipo inavyoweza kuisaidia jamii kwa namna moja ama nyingine.
Mhe.Nawanda, Mhe.Massele na Mhe. Makamba tunashukuru kwa Mchango wenu juu ya Fursa zinzopatikana,
ReplyDeleteKwa pamoja twenzetu!!!
Swali:Kwa nini viongozi wetu hawatumii lugha ya taifa(Kiswahili)kuhutubu kwenye makongamano ya kimataifa ?Nahisi sababu kiingereza sio lugha yetu hivyo wenye lughe yao hupata taabu sana kutuelewa,mfano wa baraza la umoja wa mataifa -NY.
ReplyDeleteMh. Rais angetumia kiswahili ingekuwa vizuri sana kama wale wa nchi nyingine wanavyotumia lughe zao.
Maana pia kwa kutumia lughe yako utaweza kueleza yale maoni yako kirahisi na kukabidhi hiyo hutuba kwa lugha ya kiingereza.