Na Edwin Moshi, Makete
Serikali wilayani Makete mkoani Njombe imewataka wananchi kutoa ushirikiano wa pamoja kuwakamata ama kutoa taarifa kwa ngazi husika pindi wanapowaona watu wakijisaidia ovyo maeneo yasiyo rasmi
Hayo yamesemwa na afisa afya wilaya ya Makete Bw Boniphace Sanga wakati akizungumza na mtandao huu na kuongeza kuwa kumekuwa na ongezako la magonjwa hasa ya kuhara ambayo yanatokana na watu wanaojisaidia ovyo na kuchafua mazingira
Bw sanga amesema jukumu la usafi ni la kila mmoja na si la bwana ama bibi afya pekee na kwa kuwa wananchi ndio wanaoshinda maeneo mbalimbali wanawaona wale wanaojisaidia hovyo na kuomba watoe taarifa kwenye ofisi yake ili wachukuliwe hatua za kisheria
Amesema inashangaza kuona hadi sasa wapo watu ambao hawana vyoo na wanaongoza kwa kuchafua mazingira kutokana na kujisaidia ovyo, na kutoa wito kuwa msimu huu ni wa kiangazi hivyo wanatakiwa kujenga vyoo kabla mvua haijanyesha
"Kwa kweli natoa wito nyumba bila choo haijakamilika, acheni kun***a(akimaaisha kujisaidia) maeneo ambayo si kwa ajili hiyo, unakuta mtu kavaa vizuri lakini ni namba moja kujisaidia maporini, huu si ustaarabu na watu wa namna hii ndio wanaoleta magonjwa kwenye wilaya yetu
Katika hatua nyingine Bw. sanga amewaomba wananchi kuendelea kujijengea utaratibu wa kutupa taka maeneo yanayoruhusiwa( kwenye vizimba vya taka) na kuwaasa kuacha tabia ya kutupa chupa za soda na maji mitaani kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokamatwa


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...