Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya
akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma mpya ya Airtel Yatosha
inayomwenzesha mteja wa Airtel kupata kifurushi cha maongezi , sms na
internet na kuwasiliana na mitandao yoyote nchini, sasa kwa shilingi
499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja na kifurushi cha internet
cha 125MB.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza kuboresha
vifurushi vyake vya huduma ya Airtel yatosha hivyo kuvifanya kuwa
bora, vya ushindani na gharama nafuu nchini.
Akiongea kuhusu kuboreshwa kwa huduma hiyo , Mkurugenzi wa mawasiliano
wa Airtel Bi, Beatrice Singano Mallya alisema "huduma ya Airtel
Yatosha inaendelea kutosha kuliko yoyote nchini! sasa vifurushi vya
Airtel yatosha vya siku zimeendelea kuboreshwa na kuwa vya gharama
nafuu zaidi, kwa shilingi 499 mteja anapata dakika 20, sms 300 pamoja
na kifurushi cha internet cha 125MB. Bei ni poa na ya gharama nafuu
ukilinganisha na huduma nyingine za vifurushi zinazotelewa sokoni"
Bi Singano alisema Sambamba na hili vifurushi vya Airtel yatosha
vinamuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote ule nchini
wakati wowote masaa 25 yaani mteja anafaidika na vifurushi hivi kwa
masaa 24 na 1 la nyongeza siku saba za wiki.
Kikubwa na kizuri zaidi mteja anapojiunga na vifurushi hivi anapata
nafasi ya kuingia kwenye promosheni yetu kabambe ya Airtel Yatosha
Shinda Nyumba na kujishindia pesa taslimu au nyumba za kisasa
zilizoko Kigamboni jijini Dar es saalam".
"Airtel inaendelea na dhamira yake ya kuboresha huduma zake ikiwemo
Airtel money yatosha pamoja na vifurushi vya Airtel yatosha vilivyo na
gharama nafuu na kukuwezesha kuwasiliana kwa gharama nafuu zaidi ndani
na nje ya nchi". aliongeza mmbando.
Kujiunga na vifurushi mbalimbali vya Airtel yatosha mteja anatakiwa
kupiga *149*99# na kuchagua kifurushi kinachokithi mahitaji yake.
Airtel yatosha inapatikana katika vifurushi vya siku, wiki au mwezi
na vifurushi vyake vinadumu kwa masaa 25 kwa siku.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...