Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kufanya kikao na Menejimenti ya NIDA Septemba 18,2013. Dk. Nchimbi katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil na Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi. Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa Ujenzi wa Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu na zoezi la Usajili wa watu linaloendeshwa na NIDA ikishirikiana na Serikali za Mitaa, Uhamiaji, RITA na Vyombo vya Usalama.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Ndugu Dickson Maimu, akimkaribisha Mhe Waziri
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akieleza jambo menejimenti ya NIDA, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, kushoto ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Katika Operesheni za Karne hapa nchini ambayo tutamkumbuka sana Mhe. Raisi Kikwete na Mhe.Waziri Dr. Nchimbi ni Operesheni 'Kimbunga' ambayo imewatoa kamasi watu sio mchezo.

    ReplyDelete
  2. Jamani hizo banners zifanyeni ziwe simpo na zenje meseji fupi, watanzania sio wasomaji hizo stori ndefu wekeni kwenye vipeperushi acheni kuwa wabishi tuachieni wenye fani tufanye kazi zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...