Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi ametembelea Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kufanya kikao na Menejimenti ya NIDA Septemba 18,2013.
Dk. Nchimbi katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil na Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo, Haji Janabi.
Lengo la ziara hiyo ni kufuatilia utekelezaji wa Ujenzi wa Mfumo wa Utambuzi na Usajili wa Watu na zoezi la Usajili wa watu linaloendeshwa na NIDA ikishirikiana na Serikali za Mitaa, Uhamiaji, RITA na Vyombo vya Usalama.
Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Ndugu Dickson Maimu, akimkaribisha Mhe Waziri
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akieleza jambo menejimenti ya NIDA, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu, kushoto ni Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abduwakil.
Katika Operesheni za Karne hapa nchini ambayo tutamkumbuka sana Mhe. Raisi Kikwete na Mhe.Waziri Dr. Nchimbi ni Operesheni 'Kimbunga' ambayo imewatoa kamasi watu sio mchezo.
ReplyDeleteJamani hizo banners zifanyeni ziwe simpo na zenje meseji fupi, watanzania sio wasomaji hizo stori ndefu wekeni kwenye vipeperushi acheni kuwa wabishi tuachieni wenye fani tufanye kazi zetu.
ReplyDelete