Wachezaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto), Nadir Haroub (Canavaro), wakiwania mpira katika lango la Ruvu Shooting, wakati wa mchezo wa Ligi kuu ya soka Tanzania bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 1-0. (Picha na Francis Dande)
Simon Msuva (kushoto) 
 Mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu akichuana na beki wa Ruvu Shooting, Shaban Suzan.
 Golikipa wa Ruvu Shooting, Abdul Seif akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni mwake.
 Furaha ya ushindi......Wachezaji wa Yanga, wakishangilia balo lililofungwa na Mrisho Ngasa.
 Simon Msuva akichuana na beki wa Ruvu Shooting.
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa akimtoka beki wa Ruvu Shooting, Stephano Mwasika, ikiwa ni mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya timu yake hiyo ya Jangwani kumlipia faini ya shilingi milioni 45 alizokuwa anatakiwa kulipa kwani alisaini Simba SC pia hivyo kumfungia mechi sita na kumtaka arejeshe Sh. Milioni 30 alizopewa na Simba pamoja na  na fidia ya Sh. Milioni 15.
 Mshambuliaji wa Ruvu, Shooting, Ayoub Kitala akimiliki mpira huku akizongwa na mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa. Kushoto ni Cosmas Lewis

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sikuwepo uwanjani lakini kwa mujibu wa TBC taifa, mfungaji sio Ngasa ni Kiiza. Hata web site ya Yanga imeripoti hivyo.

    sesophy

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...