Moja ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Bi Angela Aloyse, akishika mfano wa titi lenye dalili za awali za ugonjwa wa saratani ya matiti unavyo kuwa kwa Mwananmke. Hospitali ya Aga Khan iliendesha zoezi la upimaji wa saratani ya matiti na shingo ya uzazi katika viwanja vya Mlimani City, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii, Mamia ya wakazi wa jiji hilo walijitokeza kupata huduma hiyo iliyokuwa ikitolewa bure. Pamoja nae katika picha ni muuguzi kiongozi wa Hospitali ya Aga Khan Lucy Hwai.
Muuguzi kiongozi wa hospitali ya Aga Khan Bi. Lucy Hwai akitoa elimu juu ya ugonjwa wa saratani ya matiti na shingo ya uzazi kabla ya kupata vipimo kwa baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kupima ugonjwa huo mwishoni mwa wiki hii. Mamia ya wakazi wa jiji hilo walijitokeza kupata huduma hiyo iliyokuwa ikitolewa bure na Hospitali hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...