Mkurugenzi wa Shirika la AMREF Tanzania Dkt. Festus Ilako (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga kupitia kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania” siku ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hiyo. Kushoto ni Mkurgenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy Mapunda, kulia ni Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso.
 Makamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki M, Jacqueline Woiso (kulia) akisisitiza jamii nzima juu ya kutambua umuhimu wa kuwasomesha wakunga nchini ambapo azma hiyo itafanikiwa kwa kuunga mkono kampeni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako.
 Mkurgenzi Mtendaji wa kampuni ya Montage Teddy Mapunda (kushoto) akiwashukuru washirika wanaoendelea kuunga mkono kameni ya “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”, baadhi ya washirika hao ni ITV/Radio One, Clouds Media Group, Banki Kuu Tanzania (BOT), Serena hoteli, benki ya NBC, Toyota Tanzania Tanzania One, DSTV, PPF, TACAIDSWHO na MSD. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la AMEF Tanzania Dkt. Festus Ilako.
Baadhi ya waandishi wa habari na washiriki wa mkutano unaohusu chakula cha hisani cha kuchangisha fedha kwa ajili ya kusomesha wakunga uliofanyika leo jijini Dar es salaam. Kampeni ya kuchangisha fedha inaongozwa na kauli mbiu inayosema “Simama kwa ajili ya mwanamke wa Tanzania”. Chakula hicho cha hisani kitafanyika siku ya Ijumaa Oktoba 11, mwaka huu, Mgeni rasmi atakuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ataongoza uchangiaji wa fedha kwa ajili ya kampeni hiyo. (Picha zote na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...