Mamia ya wananchi wa Chato wamekusanyika kwa wingi kushuhudia uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyojengwa kwa ufadhili wa Ubalozi wa Japan na kwa kushirikiana na wananchi wa Chato.

Uzinduzi huo ambao ulifanywa na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada na Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Seif Rashid ulidhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga ambao ndio walikuwa wa wakandarasi wa wodi hiyo kupitia SUMA JKT na waziri wa ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Chato.

Akimkaribisha Balozi wa Japan kuongea na wananchi wa waziri Magufuli alimpongeza Balozi huyo wa Japan kwa misaada mbalimbali wanayoipatia Wilaya ya Chato ambapo amesema mbali na ujenzi wa wodi hiyo ubalozi wa Japan pia umewahi kufadhili ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Nyamirembe, shule ya msingi Bwanga na shule ya kidato cha tano na sita ya Chato na misaada mingine katika idara ya Afya.

Naye Balozi wa Japan akiongea na wananchi wa Chato aliupongeza uongozi wa Wilaya na mbunge wa Chatop Dkt. John Pombe Magufuli kwa kusimamia vyema jengo hilo ambalo limekamilika kwa kipindi kifupi cha miezi 5 ambapo yeye alitarajia litakamilika miezi 12.

Balozi huyo amesema ataendelea kushirikiana na Wilaya ya katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Chato.

Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid amewaasa wananchi wa Wilaya ya Chato kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya ili changamoto wanazokumbana nazo ziweze kutatuliwa.

Amesema kwa mwaka huu wizara ya Afya itaajiri watumishi wapatao 11,000 ili kupunguza tatizo la uhaba wa watumishi wenye vituo vya Afya na hospitali.

Wodi hiyo iliyoanza kujengwa mwezi Machi 2013 imegharimu jumla ya sh. 216,897,296/= kiasi cha Shilingi milioni mia moja tisini na mbili (192,357,296) zilizotolewa na Ubalozi wa Japan na Sh. 24, 540,000/= zimechangiwa na Halmashauri ya wilaya ya Chato na nguvu za Wananchi.
Waziri wa ujenzi na mbunge wa jimbo la Chato Mhe. Dkt. John Magufuli akiongea na wananchi wa Chato kwenye uzinduzi huo.
Balozi wa Japan Masaki Okada akiongea na mamia ya wananchi wa Chato.
Kikundi cha ngoma cha Bujora kikitoa Burudani wakati wa Uzinduzi.
Balozi wa Japan katika picha ya pamoja na viongozi walioshuhudia uzinduzi huo waliokaa kutoka kulia ni Katibu tawala Mkoa wa Geita Mhe. Severine Kahitwa, Naibu katibu Mkuu wizara ya Ujenzi, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Seif Rashid, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Magufuli, Balozi wa Japan Mhe. Masaki Okada, Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo na waliosimama kamati ya usimamizi wa ujenzi wa wodi.
Balozi wa Japan katika picha ya pamoja na viongozi walioshuhudia uzinduzi huo waliokaa kutoka kulia ni Katibu tawala Mkoa wa Geita Mhe. Severine Kahitwa, Naibu katibu Mkuu wizara ya Ujenzi, Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt. Seif Rashid, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Magufuli, Balozi wa Japan Mhe. Masaki Okada, Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Meja Jenerali Raphael M. Muhuga na Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo na waliosimama Viongozi wa Suma JKT ambao ndio walikuwa wakandarasi wa wodi hiyo.
Wananchi wakiwa ndani ya hospitali ya Wilaya ya Chato wakitoka kushuhudia uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...