Na Richard K. Bagolele
Balozi wa Japan nchini Tanzania Bw.Masaki Okada Anatarajia kuzindua wodi ya akina mama katika hospitali ya wilaya ya Chato mnamo tarehe 22/10/2013.
Katika uzinduzi huo Balozi wa Japan ataambatana na Waziri wa ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe. John Pombe Magufuli na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Hussein Mwinyi.
Wodi hiyo iliyoanza kujengwa mwezi Machi 2013 imegharimu jumla ya sh. 216,897,296/= kiasi cha Shilingi milioni mia moja tisini na mbili (192,357,296) zilizotolewa na Ubalozi wa Japan na Sh. 24, 540,000/= zimechangiwa na Halmashauri ya wilaya ya Chato na nguvu za Wananchi.
Ombi la ujenzi wa wodi hiyo ya kuhudumia akina mama na Watoto liliwasilishwa na Mheshimiwa Magufuli wakati alipokutana na Balozi Okada mwanzoni mwa mwaka 2012.
Balozi huyo wa Japan mara baada ya kupokea maombi hayo alituma maafisa wake kukutana na Watendaji wa Halmashauri ya Chato na baadaye kuikagua Hospitali hiyo inayohudumia zaidi ya watu laki tano (500,000) katika wilaya ya Chato.
Balozi wa Japan hapa nchini, Mheshimiwa Masaki Okada kwa pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmshauri ya Chato Bw. Shaaban Ntarambe walisaini hati ya makubaliano ya kuchangia ujenzi wa wodi hiyo katika hafla fupi iliyofanyika Ubalozi wa Japani, jijini Dar es Salaam mwezi Machi 2013.
Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Rodrick Mpogolo akiweka jiwe la Msingi kwenye wodi hiyo tarehe 15/10/213.
Mwonekano wa Mbele wa Wodi mpya ya akina mama Hospitali ya Wilaya ya Chato.
sehemu ya ndani ya wodi ya akina mama iliyojengwa na Ubalozi wa Japan kwa kushirikiana na Halmshauri ya Wilaya ya Chato.
sehemu ya ndani ya wodi ya akina mama inayotarajiwa kufunguliwa na Balozi wa Japan nchini Tanzania tarehe 22 Oktoba, 2013.
mwonekano wa Hospitali ya Wilaya ya Chato




SAMAHANI MKUU,WILAYA YA CHATO IKO MKOA GANI?
ReplyDeleteNani kasema wilaya tena. Ukijibiwa utauliza wilaya ya ubungo na kawe ziko mkoa gani!!! Tehe tehe teheeeeeeeeeee
ReplyDeleteChato iko Biharamulo, Kagera, kanda ya Ziwa
ReplyDelete