Balozi wa Marekani Nchini, Alfonso E. Lenhardt leo Agosti Mosi, 2013, amezuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kuiaga Menejimenti ya Wizara.
Akizungumza na Menejimenti amesema idara za Wizara hiyo ambazo ni pamoja na Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto, Wakimbizi, Huduma kwa Jamii na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa zinafanya kazi nzuri ya kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

Amesema yeye na familia yake kamwe hawataisahau Tanzania kwa sababu walipata makaribisho mazuri na wameishi kwa amani na huku kukiwa na ushirikiano mzuri kutoka kwenye vyombo vya usalama.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi amemshukuru Balozi Lenhardt kwa ushirikiano na mchango mkubwa wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo chini ya Wizara hiyo na idara zake aliokuwa akitoa kutoka nchini mwake.

Amesema ana amini Balozi ajaye atakuwa na ushirikiano mzuri na Wizara yake na Serikali kwa ujumla.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamani kuaga miezi saba? Hamalizi kuaga! Kila siku!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...