Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bibi.Ritva Reinikka muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kushoto ni Bwana James Adam Makamu Mstaafu wa Benki ya Dunia.
Wakati wa Mkutano huo uliowashirikisha pia Wajumbe wengine kutoka serikalini na Benki hiyo viongozi hao walijadili kwa kina Mpango wa Kunusuru kaya Maskini kupitia mpango wa TASAF III.
Madhumuni ya Mpango huu ni kuziwezesha kaya maskini kuongeza kipato,fursa na kuimarisha lishe.Walengwa wa mpango huu ni kaya ambazo zinaishi katika umaskini mkubwa katika mazingira hatarishi vijijini na katika shehia upande wa Zanzibar.
Mpango huu utatekelezwa katika kipindi cha miaka 10 chenye awamu mbili za miaka mitano kila moja.Bajeti ya utekelezaji wa mpango huu ni kiasi cha Dola za Marekani million 272.9.Mchango wa fedha hizo utatolewa na wadau mbalimbali ikiwemo Serikali ya Tanzania amabyo itachangia kiasi cha Dola za Marekani millioni 30, Benki ya Dunia Dola Za Marekani Millioni 220, DFID Dola za Marekani 16,Serikali ya Hispania Dola za Marekani 6, na Shirika la Misaada la Marekani(USAID) itachangia kiasi cha Dola za Marekani 900,000

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hizi pesa zinazosaidia kaya maskini za TASAF ni vizuri kuelewa uendelevu wake ni za mkopo au msaada?

    ReplyDelete
  2. Je pesa kama hizi zinaweza kutumika kama social security za wasiokuwa na ajira kwa muda ili waweze kujimudu kama nchi zilizoendelea zilipoamua kusaidia wale waliopoteza kai miaka ya sitini kwa sababu ya mashine na viwanda kuchukua kazi zao, au kwa nchi kama yetu haiwezekani, uwezo wa kifedha kama huo aupo...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...