Bofya mshale usikie sehemu ya sauti ya mwanadada baada ya watu wawili wanaotuhumiwa kuwa ni wezi a.k.a Wapigaji/Matapeli kukamatwa usiku huu kwenye hoteli ya Piccolo Beach,Kawe jijini Dar es Salaam.

Watu hao ambao wamekamatwa ni Bw. Takula Mayenga mkazi wa Mbezi Temboni na Bw. Juma Hamis ambaye ni mkazi wa Tabata wakiwa na nyaraka tofauti ikiwemo kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa, kadi za benki pamoja na simu zaidi ya kumi,wakiwa katika harakati za kumtapeli mwanadada mmoja aliejitambulisha kwa jina la Rebecca ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara cha CBE,Mkazi wa Mbezi Beach jijini Dar es Salaa  .

Akisimulia tukio dada huyo ambaye alipatwa na tukio hilo la kutapeliwa Ijumaa ya wiki iliyopita alisema kuwa, ilikuwa ni Ijumaa iliyopita wakiwa wamekaa katika fukwe wakipunga upepo ndipo alipokuja tapeli huyo na kukaa nao na baadae aliwawekea madawa ya kulevya na kuondoka na dada huyo kwenda kumtupa baharini.
Mtuhumiwa  mmoja wa Uwizi aliejitambulisha kwa jina la Juma Hamis alikutwa na  Kitambulisho  kinachoonesha kuwa ni cha Kazi cha Idara ya Usalama wa Taifa chenye jina la Kenedy Magige,akiwa amewekwa chini ya Ulinzi mara baada ya kunaswa Usiku huu kwenye Hoteli ya Picolo,Kawe jijini Dar es Salaam,
 
 Watuhumiwa hao wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Maelezo ya huyo mdada yu hodari, safi sana.

    ReplyDelete
  2. Pamoja na picha kuwa nyingi lakini sura zao hazionekani kabisa

    ReplyDelete
  3. Mlio na vitambulisho halali vya TISS, mnasemaje kuhusu kitambulisho hicho? Ndivyo vitambulisho vyenu vinavyoonekana? Napenda kujua ili siku nyingine na mimi nikionyeshwa na wajanja a.k.a wapigaji nipige ngoro.

    ReplyDelete
  4. Am not surprised, its part of corruption in Tanzania

    ReplyDelete
  5. Mapinduzi mimi nilishawahi kukiona mahali cha halali. kiko hivyo bali hiki wekundu wake ni tofauti kidogo na nilichokiona rangi ile yaitwa DAMU YA MZEE

    ReplyDelete
  6. Muuuuuuuh kwa kweli nchi hiyi kiboko.

    ReplyDelete
  7. michuzi kama kweli ulikua unataka watu wawajue na wajihadhari na hawa watu mbona hujatoa sura zao waonekane.mbona haki ngowi katowa sura zao na kila kitu ili tujue tujihadhari vipi tukiona tena sura kama hizi.hii inasaidia kwa mtu yeyote na kwa namna yeyote.usiwe unafanya hivi.siku mpaka yawakute nyinyi ndio utaweka sura yao.ukiweka story yeyote uwe unaweka kwa kufundisha au kwa kutahadharisha,inakuwa poa.hivi ulivyofanya ni kama hutaki wajulikane ili waendelee kuibia watu.ni hayo tu hata ukiibania wewe uliesoma tu inatosha utakua umejifunza chochote.

    ReplyDelete
  8. Ugumu wa maisha kipimo cha akili lakini sio hadi kwenye Taaluma nyeti kama za Usalama!

    Bora mara zooote ukikamatwa na Afisa yeyote wa Usalama mwambie twende Kituoni nikalipe Faini na sio Rushwa ama mapatano yoyote!

    Duhhh hadi na gari aina ya Toyota Prado?

    Afadhali wangeishia kwenye ngazi ya Upelelezi wa kawaida.

    ReplyDelete
  9. Ahhh Washikaji masihara haya?

    Vipara vikibwaaa vichwani vinawakaaa kama nini, huku mnaendesha Toyota Prado TdX kumbe kazi yenu Utapeli, Usanii na Wizi!, si bora mngepaki Kijiweni Kituo cha basi mkawa mnakodisha kama Teksi bubu Shs, 10,000/= kwa Elfu Kumi majiko yenu nyumbani yasingelala paka na watoto wenu wangeweza kwenda choo?

    ReplyDelete
  10. Duhhh Kipigo cha Polisi baada ya Wizi hadi picha ya tano (5) kutoka juu suruali limevuka na Lichupi la misitari misitari nje linaonekana?

    ReplyDelete
  11. Washikaji Maisha hayahitaji mabavu kwa saana kama mlivyofanya kufikia kujipachika Uafisa wa Usalama wa Taifa!

    Hivi kweli na ji Toyota Prado lenu hilo navitambi vyenu na vipara kichwani mngeegesha Kituo chochote cha Madala dala mkabeba abiria wanaoshuka kuingia njia za ndani mngekosa kula?

    ReplyDelete
  12. Ahhh majanga mbona majanga?

    Wake zao masikini kila siku wapo majumbani Waume wanatoka majumbani kwenda kazini na wanaingi majumbani wakirudi kutoka kazini.

    Wanapaki magari wanapokelewa mazaga zaga waliyonunua.

    Kumbe eee siri ya mtu ni Kichaka!, KAMA PASSWORD YA MTANDAO, NAMBA YA SIRI YA M-PESA, AMA YA AKAUNTI YA BENKI AMBAYO ANAIJUA MUHUSIKA.

    Wake zao wakikarangiza majumbani kumbe Waume zao ni wezi wa Mujini?

    ReplyDelete
  13. Masikini weee Vijana Kazi ya Upolisi wanaipenda ni vile kilicho waponza ni kufanyia ''Manyasini'' na kinyume na Sheria.

    Mhe.IGP Mwema umewaona vijana hao?,,,wanayo ari ya kazi lakini njia waliyotumia siyo.

    Muwaadhibu kwa Kosa lao hili halafu na wakitoka kwa uchache muwaingize Kundini Idara ya Usalama wawe na kazi angalau kuwa Mainfoma!!!

    ReplyDelete
  14. Ikiwa kazi ni uwizi basi hata hiyo gari ni ya wizi ichunguzwe kwa makini itagundulika ni ya wizi kwani bongo kwa wizi kumezidi mpaka hata sipapendi naona bora nifie huku ugenini maana mtu huna amani ukisema unatoka kufresh mind basi ishakua balaa saasa tufanyaje hata hii hali ikome watu kufanya halali hawataki wanataka utajiri wa haraka kwa kurudisha wenzao nyuma dawa yao hao ni kifo tuu

    ReplyDelete
  15. Jamani sio gari lao hilo ni la utapeli pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...