Mwenyekiti wa CCM mkoa wa IringaNdugu Jesca Msambatavangu akiwaongoza viongozi wa vyama vya ukombozi mara tu walipowasili mkoani Iringa kwa ziara ya siku moja ya kutembelea chuo cha Ihemi, Viongozi hao wapo nchini kuhudhuria mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vya Ukombozi utakaofanyika tarehe 9,Septemba 2013 jijini Dar es salaam.
Viongozi mbalimbali kutoka vyama vya ukombozi wakifurahia ngoma za asili wakati walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa nduli tayari kwa ziara ya siku moja kukitembelea chuo cha Ihemi.
Viongozi kutoka vyama vya Ukombozi Afrika wakionyesha ishara ya mshikamano wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwakaribisha rasmi kwenye chuo cha Ihemi mkoani Iringa. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...