Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE),Bw. Almas Maige (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza kuanza kwa Mchakato wa kumpata Mwajiri Bora kwa kipindi cha Mwaka 2013.Tuzo ya Mwajiri Bora wa Mwaka (Employer of the Year Award - EYA) ni tukio ambalo limekuwa likifanywa kila mwaka na Chama hicho kwa mujibu wa kalenda ya Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Tuzo imelenga kuwezesha uwapo wa namna bora kabisa ya kusimamia raslimali watu, kitaaluma na kimazingira kwa nia ya kuleta Tija na utendeji bora mahala pa kazi.Wengine Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Chama hicho,Dr. Aggrey Mlimuka (kulia) na Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa ATE,Bi. Joyce Nangai.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...