Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk. Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja itakayioanza Oktoba 7. Kushoto ni Meneja wa tawi la Premier, Fabiola Mussula.

DAR ES SALAAM, Tanzania

Benki ya CRDB imezinduzi wiki maalum ya Huduma kwa Wateja ‘CRDB Bank Customer Service Week’ itakayoanza kuanzia Oktoba 7 ambapo viongozi wa benki hiyo watakuwa katika matawi na kusikiliza kero mbalimbali za wateja.

Wateja watakaofika mapema na kuhudumiwa katika matawi ya benki ya CRDB watapata zawadi mbalimbali ambapo benki ya CRDB imeaandaa fomu maalum kwa ajili ya wateja kutoa maoni yao kuhusu maeneo ambayo wangependa yaboreshwe katika utoaji wa huduma.

Wateja watakaojaza fomu hizo na kutoa maoni au changamoto nzuri watajishindia safari ya siku tatu kwenda visiwani Zanzibar ambayo italipiwa na benki ya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dk.Charles Kimei amesema kuwa CRDB inaongozwa na kauli mbiu yake “The Bank that Listens”.

“Katika kuendelea kuutambua mchango wa wateja watu, katika wiki hii ambayo imepewa kauli mbiu ya “Je Umesikilizwa?, ambayo inalenga kuwapa nafasi wateja kuongea kwa ukaribu na viongozi wa matawi na kutoa maoni yao jinsi gani wangependa wahudumiwe” alisema Kimei na kuongeza kuwa katika wiki hii viongozi wa juu wa benki watakuwa wakifanya kazi katika matawi yaliyopo jijini Dar es Salaama katika mikoa mingine, pia fulsa hiyo itatumiwa na wateja kufahamiana na viongozi wa juu wa benki hiyo.

Benki hio imekuwa kinara wa kuingiza sokoni bidhaa bunifu zenye kukidhi mahitaji ya wateja kama vile mikopo mbalimbali inayolenga kuboresha maisha na biashara zao.

Kusogeza huduma karibu zaidi na wateja kupitia njia mbalimbali kama vile FahariHuduma (Agency Banking)
Kuongeza njia za kutolea huduma, ikiweomo utumiaji wa njia mbadala za kutolea huduma yaani “altenative Banking Channels” ikiwemo utoaji wa huduma kupitia simu za mkononi yaani SimBanking, utoaji wa huduma kupitia mtandao yaani Internet Banking, kupitia account Statement kwa njia ya mtandao yaani E-Statement, kutoa huduma kwa kutumia matawi yanayotembea (Branch Wheels)

Kuendelea kuboresha mifumo ya utoleaji huduma, sasa hivi mashine za kutolea huduma ni za uhakika zaidi na baadhi ya matawi yanatoa huduma siku zote za wiki na hata siku za sikukuu kama vile tawi la Mlimani City lililopo Dar es salaam, Vijana-Dar es Salaam, tawi la Mwanjelwa (Mbeya), Nyanza (Mwanza) na Meru (Arusha).

Pia Benki ya CRDB imeboresha vituo vya huduma kama vile Call Center ambayo hivi punde itaanza kufanya kazi kwa muda wa saa 24.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. CRDB tumewasikia,

    Naanzia hapa kutoa Maoni ama mapendekezo yangu:

    1.ATM Deposit huduma (Kuingiza Fedha kwa njia ya Mashine), ziboreshwe zaidi ama kupanuliwa kwa kuwa mara kwa mara tukifika kuweka fedha hasa siku ambazo Benki hazifunguliwi ama muda ambao Benki zimefungwa tunakuta mashine hazipokei Fedha !, kitu ambacho ni kikwazo cha Ustawi wa wateja kulazimika kukaa na marundo ya fedha mikononi.

    2.Kutoa sehemu ya Hisa kwa Wafanyakazi wenu (Kwa vile CRDB BANK PLC. imeorodheshwa ktk Masoko ya Hisa DSE, hii itasaidia zaidi Wafanyakazi wa CRDB kujisikia kuwa Benki wanaimiliki hivyo sio rahisi mtu kuhujumu anachomiliki sehemu yake, Hivyo ni wazi kwa umiliki huo Wafanyakazi watakuwa na ari ya kazi zaidi hivyo ubora wa Huduma kwa Wateja kuimarika zaidi na pia Benki kuimarika zaidi.

    3.Promosheni za Mashindano ya Benki zielekezwe zaidi ktk Asset Classes Mfano kuendesha Draw halafu mshindi kupewa zawadi ambayo ni Rasilimali ''Asset'' iliyokuwa 'more tangible and liquid' yaani yenye TIJA badala ya Mshindi kupewa Tiketi ya ndege kwenda Dubai, South Afrika ama kukaa Hotelini Zanzibar!

    Mfano wa zawadi zenye TIJA ni:

    (i)-Mshindi kupewa sehemu ya Hisa za CRDB ktk soko la Hisa la DSE.

    (ii)-Mshindi kupewa Kiwanja ama kujengewa nyumba.

    (iii)-Mshindi kufanyiwa Business development Consulting na kupewa Business plan na kufunguliwa Biashara.

    (iv)Mshindi kupewa Mafunzo Mafupi a Kozi a Ujasiriamali kama yupo ktk sekta ya Biashara ndani ya Safari atakayo kwenda Zanzibar, Afrika Kusini ama Dubai.

    (v)-Kwa ujumla zawadi za Droo zielekezwe zaidi ktk TIJA na ukuzaji kwa Mteja na sio zawadi za anasa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...