Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana wakiwa tayari kuipokea bendera ya RECSA kabla ya Dk Nchimbi kukabidhiwa bendera hiyo ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa kuliongoza baraza hilo kwa kipindi cha miaka miwili. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania
 Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wa Baraza hilo pamoja na watendaji wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na wananchi mablimbali baada ya kukabidhiwa uenyekiti huo katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.
 Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimkabidhi zawadi mwenyekiti aliyemaliza muda wake wa kuiongoza RECSA ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania.  
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia viti vya mbele) akiwa na watendaji wengine wakuu wa wizara hiyo pamoja na wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (hayupo pichani) mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana. Hafla hiyo makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo. Nchi wanachama wa RECSA ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea, Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...