Mwalimu wabshulenya msingi Makuburi Grace Kado akishukuru baada ya kukabidihiwa madawati

======  =====  ========
TFDA imekabidhi msaada wa madawati  100 kwa shule Mbili za Msingi za Makuburi Jeshini na Makuburi katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 10 ya TFDA toka kuanzishwa kwake.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Bw. Hiiti B. Sillo alisema kuwa thamani ya madawati hayo ni Sh. 17,000,000/ ambazo zimetokana na michango ya watumishi na TFDA Kama Taasisi. Aidha, Bw. Sillo alisema kuwa Sh. 600,000/ zaidi zimeelekezwa katika kukarabati darasa Moja la shule ya msingi Makuburi Jeshini.

vilevile Bw. Sillo alieleza kuwa pamoja na majukumu ya TFDA ya kulinda Afya ya Jamii, Mamlaka pia inalo jukumu la kujali na kuthamini jamii inayoizunguka kwa kuwa TFDA inaishi na Jamii na haipo kisiwani.
Hapa mwalimu Mkuu wa Makuburi Jeshini akipokea msaada wa madawati.
Watoto wa shule wakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa TFDA wakifurahia madawati.

Watoto wakijaribu kukalia madawati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwa kasi hii, Kiswahili kitafifia miak 20 ijayo!

    ReplyDelete
  2. mimi najiuliza hivi TDFA sio serikali kweli??? kwanini watoe madawati kwa makuburi tu? wengine? je hiyo hela ilikuwa ktk budget? na kwanini bunge lipitishe budget ya TFDA kununua madawati wakati inashughulikia DAwa na Chakula? au ni mimi tu nisiyeelewa? mdau

    ReplyDelete
  3. Kiswahili "kitafifia"

    Mdau no 1, fafanua mimi ni "kifimbo cheza" tatizo liko wapi ili nianze kazi yangu?

    ReplyDelete
  4. Anonymous no.2 maelezo ya hii habari inaonyesha kwamba fedha nyingine zimetokana na michango ya watumishi wa TFDA. Labda watufahamishe wafanyakazi TFDA walichanga kiasi gani na serikali nayo kiasi gani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...