Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua semina ya mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya nchini, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (zanzibar) Vuai Ali Vuai. (Picha na Bashir Nkoromo)
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu lengo la mafunzo hayo.
Katibu wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Kartibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza kwenye semina hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Dodoma, leo kwa ajili ya kufungua semina hiyo.
PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILI BOFYA HAPA.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...