Hali ilivyokuwa kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi baada ya wasafirishaji wa mabasi kufanya mgomo kufutia serikali kuondoa tozo ya asilimia tano iliyokuwa ikizidi katika mizani. Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro alifanikiwa kuwashawishi wenye mabasi kuendelea na safari baada ya masaa kadhaa
Baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi wakiwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi kuhakikisha hali ya usalama kwa abiria. Picha na Dixon Busagaga wa Globu Jamii Moshi.
Afrika taabu kila siku najiuliza nirudi au nisirudi hasa nionapo vitu kama hivi, yaani hii ni karne ya 21 bado watu wanaishi kwa kubahatisha.Kwa jinsi ilivyo hapo hao abiria hawana mbinu mbadala zaidi ya kurudi nyumbani na mabegi yao.Yaani mtu mmoja au watu wawili wanaweza kuharibu mipango ya watu elfu hiyo ndio afrika ilivyo,Hatma ya hawa abiria ipo kwa hao wenye vyombo vya usafiri.
ReplyDeleteUbabe nao umezidi bila kukaa kuelewana. Hilo suala ni la kisheria na kama ndio hivyo sheria sio kulala na kuamka na kuleta ulicho waza eti tu kwasababu una mamlaka fulani. Kwakweli watanzania tutabanwa sana katika kile kidogo tunachokipata kwa siku. Leo hii mambo ya uzito mzani yamebanwa tayari, bado mambo ya kodi ya simu kila mwezi, nk. Kwakweli watanzania tujipange kwa hilo maana kuna watu wamegeuza hii nchi ni yao peke yao.
ReplyDeletePoleni watanzania wenzagu kwa adha ya usafiri mlioipata
Ama kweli mafahali wawili wakigombana ziumeazo ni nyasi. Ona wananchi wanavyonyanyasikia bila kwa sababu hakuna nja mbadala ya usafiri.
ReplyDelete