Barua ya wazi kwa Wapendwa Watanzania
wenzangu
Kwanza
nianze kwa kuwapa pole jirani zetu na ndugu zetu wakenya kwa tukio baya kabisa
la ujasusi lilotokea mwisho wa juma lilopita. Ni jambo ya kusikitisha na lenye
kujaa na maswali mwengi ya kujiuliza. Imefika mahali kuna watu hawathamini utu
wala maisha ya binadamu mwenzake. Poleni sana ndugu zetu na tuko pamoja.
Mambo
ya kujifunza:
1. Mwenzako akinyolewa, na
wewe anza kutia maji. Ninasema hivi kwasababu tusidhani kwa sababu tupo mbali
na Somalia basi tuko salama. La hasha, hawa jamaa hawalali, na chokochoko na dalili tulianza kuziona mapema kabisa.
Tumeona matukio ya mabomu na tindikali,
na jana bomu kurushwa Zanzibar. Inatisha kabisa. Nashauri vyombo vya usalama
vifunguke macho na viache kufanya mabo kwa mazoea, tubadilike na tujifunze
mbinu mpya za kukabiliana na ugaidi. Tusione aibu kuomba msaada wa kitaalamu na
vifaa kutoka kwa wenzetu waliotutangulia kiitelijinsia
2. Somo la uzalendo ndiyo
mahali pake hapa. Mtu mzalendo hawezi kuiuza nchi yake kwa ajili ya njaa zake.
Kutokana naa umbwe la umasikini kuongezeka, inakuwa rahisi sana mtu kukubali
kushirikiana na watu wenye nia mbaya kuumiza nchi yetu. Hizo ni tama na badala
ya kutatua matatizo inazidisha maana:
a. Utalii utakufa
b. Wawekezaji wataogopa kuja
kuwekeza
c. Hata vile vichache tulivyo
navyo vitahujumiwa
d. Uhai wa kila mmoja wetu
utawekwa rehani pamoja na aliyechonga line
e. Kisiwa cha amani
kitatoweka (Mungua tupitishie mbali)
f. Tutaanza kunyoosheana
vidole kati ya kabila na kabila, dini na dini, bara na visiwani. Hatutakuwa
wamoja. Lazima tutaanza kutafuta mchawi
g. Hata wenye mali hawataishi
kwa amani,maana wao ndiyo watakaoviziwa kwanza; kama tulivyoona Westgate
Nini
cha kufanya:
1. Nakumbuka enzi za Mwalimu
kulikuwa na mabalozi wa nyumba kumikumi. Hawa watu walikuwa na nguvu sana
kwenye eneo lao. Japo ilikuwa sera ya CCM,lakini kutokana na vyama vingi, basi
tuifanye sera ya Taifa. Nakumbuka wakati wa utoto wetu ukipata mgeni lazima
utoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi. Hii ilisaidia vitu vifuatavyo:
a. Kujua mgeni ni nani,
anakaa muda gani na anashughuli gani. Ikitokea uhalifu, basi inakuwa rahisi
kupata pa kuanzia. Najua wengi mtasema mambo ya ujamaa, lakini tukumbuke ujamaa
ndiyo unaofanya tunajiona wamoja. Yes kuna mambo ambayo hayakwenda
vizuri,lakini utu na undugu viliimarika. Ukiangalia jirani zetu ambao walifuata
ubepari waligombana na kuuana, sisi tu ndiyo tulishikamana. Kuanzia nyumba kumi, kata, tarafa, wilaya, mkoa hata
taifa tulijivunia mshikamano na kila mtu alikaataa kurubiniwa kusaliti nchi
yetu
b. Pia ilisaidia mambo ya sensa.
Balozi wa nyumba kumi alijua idadi ya watu wake hata mtoto akizaliwa leo.
Kipindi cha sensa, walichokuwa wanafanya ni kuhakiki idadi, hata kama mmoja
ameenda likizo au amesafiri mjumbe anajua mtu wake hayupo.
c. Maswala ya sera za taifa
kama elimu afya na uzazi wa mpango viliwezekana kutoka na ushirikiano na
mabalozi wa nyumba kumi.
d. Mwanzoni balozi alikuwa
anajitolea, lakini kutokana na sababu za kiusalama, basi serikali iwape hata
kifuta jasho, na baadae waingie kwenye maswala ya usalama wa raia.
e. Tukishawawezesha hawa,
basi kila mgeni anayeingia kwenye eneo lake lazima ajue au ajulishwe, la sivyo
uhalifu ukitokea eneo lake yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuhojiwa.
Mwisho
nimalizie kwa kusema, kwa yaliyotokea kwa jirani zetu tusidhani sisi tuko
salama. Hii kwetu ni nafasi nzuri ya kujiweka mguu sawa. Ulinzi mipakani
iimarishwe, tuache kuweka siasa kwenye vitu vinavyohatarisha usalama wa Taifa
letu teule. Porojo za mabomu ya Arusha, Zanzibar, Tindikali nk vizifanyiwe
masihara hata kidogo. Wananchi wapewe taarifa ya kila jambo na watu wawajibike
au wawajibishwe wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao.
Mungu
ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.
Mdau G. Lyimo


Asante kwa point zako nzuri na nimejifunza mengine niliyokuwa siyajui kuhusu Tanzania.
ReplyDeleteIla kuhusu kuomba msaada kwa wageni tuwe waangalifu sana. Kwa sababu historia ya Afrika inaonyesha kwamba saa zingine kuomba msaada kwa wageni kumeongeza majanga yasiyoisha. Kwa mfano "divide and rule system" ilitawanya Afrika vibaya sana.
Mungu ibariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania.
Kutoka kwa,
dailylifeandliving.blogspot.com
Asante mdau Lyimo.Kama ulivyomalizia hapo mwish0-SIASA.Mimi nawalaumu wanasiasa wote duniani.Wanasiasa ndio wamehusika kwa njia moja ama nyingine kuchafua dunia hii ya leo.Kwanini dunia(UN) isipige marukufu viwanda vya mabomu na silaha zozote za moto tuone itakuwaje!!!!!!!!
ReplyDeleteDavid V
Silipendi hili neno 'KWA GARAMA YOYOTE ILE' Unafahamu maana yake?
ReplyDeleteHata ujumbe wako unapoteza maana.
Kwa garama yeyote ile inajumuisha matendo ya uvunjishi wa amani!!!!!
Tuwe makini na kauli zetu.
mtu mwingine anaandika 'SISI WATANZANIA TUNAFANYA / TUNAPENDA KUFANYA HIVI AU VILE. Mambo anayozungumzia ni ya kijinga sana halafu anatufunga watanzania wote kwenye huo ujinga.
Sion vizuri. usidhani watu wote ni kama wewe.
David V ninapenda sana wazo wako. Hivi kwanini kweli UN isilaani vikali viwanda vya mabomu na silaha??? Tunahitaji watu zaidi kama wewe kwenye hii dunia.
ReplyDeleteKutoka kwa,
dailylifeandliving.blogspot.com
Wazo lako zuri mdau, umetukumbusha Tanzania yetu ya zamani ambapo kila mmoja alikuwa mlinzi wa nchi na tulijifunza hivyo hata mashuleni. Naamini tutarudi huko siku mmoja ili tujivunie na kuufurahia utanzania wetu kuwa ni mahali salama kwa raia wake.
ReplyDelete