Ndugu Wananchi;
          Namshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza mwezi Septemba salama na kuwasiliana kwa kutumia utaratibu wetu huu mzuri.  Naomba radhi kuzungumza nanyi siku ya leo kwa sababu nilikuwa safari na nilirejea jioni ya tarehe 30 Septemba, 2013.   Awali nilifikiria nisiseme, nisubiri mwisho wa mwezi wa Oktoba.  Lakini, baada ya kupata taarifa ya yaliyojiri, nimeshauriwa na nimekubali angalau niyasemee baadhi ya mambo huenda itasaidia.  Niwieni radhi nisipoyasemea baadhi ya mambo siyo kwa kuyapuuza, bali kwa kuepuka hotuba kuwa ndefu mno.  Nitayatafutia mahali pengine pa kuyasemea.
Uhusiano na Rwanda
Ndugu Wananchi;
          Katika hotuba yangu ya mwisho wa mwezi wa Julai, nilizungumzia hali ya uhusiano wetu na Rwanda kutokuwa mzuri na tatizo la ujambazi na wahamiaji haramu katika Mikoa ya Kigoma, Geita na Kagera.  Nafurahi kusema kuwa kwa yote mawili kuna maendeleo ya kutia moyo.
          Tarehe 5 Septemba, 2013, nilikutana na kuzungumza na Mheshimiwa Rais Paul Kagame wa Rwanda mjini Kampala.  Tuliitumia fursa ya ushiriki wetu katika Mkutano wa Nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia uhusiano baina yetu na nchi zetu.  Mazungumzo yalikuwa mazuri na sote tulikubaliana kuwa yaliyopita si ndwele tugange yajayo.  Kwa sababu hiyo tulielewana kuwa tutengeneze mazingira yatakayosaidia kutuliza hali na kurudisha nchi zetu katika uhusiano mwema kama ilivyokuwa siku zote.  Nawaomba ndugu zangu hususan wanasiasa, watumishi wa umma, wanahabari na wenye mitandao ya kijamii na blog na wananchi kwa ujumla tusaidie kuimarisha uhusiano mwema baina ya Rwanda na Tanzania na watu wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Asante sn muheshimiwa Rais kwa hekima zako,mbuzi tulikua tunamla sote kwa pamoja tena kwa utulivu wa hali yajuu,ghafla anatokea mtu eti huyo mbuzi katiwa sumu,jibu kapewa palepale huyu hana sumu na tunamla mpaka aishe,mungu yupo pamoja nasi na analipenda sn TAIFA letu la TANZANIA,kaeeni mezani tumalize hivi vijitofauti mbona vidogo sn why not,,ila huyo muongo ashindwe yeye,Naitwa mdudu kakakuona,nipo UINGEREZA au uk,amani kwenu woote huko nyumbani nawapendeni sn,

    ReplyDelete
  2. Mh Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tunashukuru kwa busara zako zilizotukuka.Kwa ufupi watanzania watakukumbuka.Kuna Mambo mengi sana umefanya na matokeo yake yako mbioni ukishastaafu.Nimepitia website ya Taifa na sikuamini nilichokiona.sasa maendeleo yataonekana huo uwavi na Elimu kwa wananchi wanaoweza kuelewa umuhimu wake labda ni sisi tunaokaa nje au kidogo na nchi kama Rwanda.Wapinzani wanaotafuta muafaka kwa vurugu kwanza watambue sisi watanzania ni nje na interest zetu ila pia washerehekee uhuru wao kwa kukukumbuka Baba umewatoa mbali enzi za mzee Mkapa. Gog bless you. Ni mdau UK -SINA CHAMA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...