Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache kuwashukuru Watanzania kwa kuwa kitu kimoja na kuwezesha kufanikisha kuchangisha fedha kipindi cha wiki moja na kuwezesha kumsafirisha marehemu Tanzania kwa mazishi pia Balozi Mulamula aliwakilisha rambi rambi ya Mhe. Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara kwa wafiwa.
Mtoto wa marehemu, Joseph Kassuwi akiwaeleza Watanzania waliofika kwenye Ibada ya mpendwa mama yake maneno aliyoambiwa na mama yake kabla ya pumzi yake ya mwisho alisema mama yake alimuambia amtunze mdogo wake kabla hajamalizia alishindwa kujizuia akaanza kububujikwa na machozi na kufanya watu waliofiak kanisani hapo nao kushindwa kuvumilia.
Familia ya marehemu wakiwasha mshumaa kwa pamoja wakati wa chakula cha pamoja.
Mhe. Balozi Liberata Mulaula pamoja na maafisa Ubalozi na Rais wa Watanzania DMV wakifuatilia Ibada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. pole sana Kaka najua ningumu lakini kumbuka kunaye Mungu ataonyesha njia.

    ReplyDelete
  2. Pole sana kaka .

    ReplyDelete
  3. Poleni sana jamaani....yaani unasikitisha mno Bwana awafariji!
    Pole sana na Mungu akusaidie uweze kuwatuza hawa wototo.....Pole sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...