Moja ya kampeni dhidi ya Kifua Kikuu nchini Tanzania
Ripoti mpya ya WHO kuhusu ugonjwa Kifua Kikuu iliyotolewa jana Jumatano imeonya uwezekano wa kutoweka mafanikio yaliyopatikana kwenye tiba dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Hofu hiyo inatokana na uwezekano wa wagonjwa Milioni Tatu duniani kote kuwa nje ya mifumo ya tiba na janga la Kifua Kikuu sugu kuendelea. NchiniTanzaniamafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kupungua kwa maambukizi mapya miongoni mwa vijana lakini kuna changamoto.
Je ni zipi hizo? Assumpta Massoi wa Idhaa hii alizungumza kwa njia simu na Kaimu Mkuu wa mpango wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini Tanzania Dokta Deus Kamara ambaye kwanza anaanza kwa kueleza jipya waliloliona kwenye utafiti wa hivi karibuni ambapo takwimu za makadirio ya wagonjwa ni za chini kuliko hali halisi.
Kusikiliza alichokizungumza Dk. Kamala bonyeza hapa
http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/2013/10/idadi-ya-wagonjwa-wa-kifua-kikuu-tanzania-ni-kubwa-kuliko-makadirio-dkt-kamara/
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...