Jeshi ya Polisi Tanzania na TCCIA zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya ulinzi, usalama na ulinzi wa maisha na mali.

Akizungumza kabla ya kusaini hati hiyo Kaimu Inspekta Generali na Kamishna wa Polisi Tanzania,CP. Paul Chagonja alisema makubaliano haya ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano yaliofikiwa wakati wa mkutano wa Smart Partnership.

Alisema jeshi la polisi likotayari kushirikiana na sekta binafsi katika kuboresha mazingira ya biashara nchini na kwa kufanya hivi ni lazima kushirikiana na wadau kama TCCIA na wengine katika sekta binafsi.

Alisema Jeshi la polisi litashirikiana na TCCIA kuhakikisha masuala ya ulinzi na usalama wa mali zao yanapewa kipaombele na kuhakikisha sheria zilizowekwa zinafuatwa kikamilifu bila ya kuwa kikwazo katika biashara.

Aidha kwa upande wa Rais wa TCCIA Muhandisi Peter Chisawillo alisema kwamba wakati umefika kwa sekta binafsi kuongeza ushirikiano na jeshi la polisi ili kuhakikisha kuna usalama, amani, ustawi na utulivu wa kisiasa kwani hivi ni rasilimali muhimu katika maendeleo ya biashara na uchumi kwa ujumla.

Alisema TCCIA itahakikisha wanachama wake wanazingatia sheria na taratibu katika ufanyaji biashara zao na kwamba haya yatafanywa na ofisi za TCCIA mikoa yote ya Tanzania bara.
Kaimu Inspekta Generali na Kamishina wa Polisi Tanzania,CP. Paul Chagonja akizungumza umuhumu wa ushirikiano wa jeshi la polisi na wafanyabiashara wakati wa kusaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture aliyekaa Kushoto kwake ni Rais wa TCCIA Eng. Peter Chisawillo na Mkurugeszi Mtendaji wa TCCIA Daniel Machemba.
Kaimu Inspekta Generali na Kamishina wa Polisi,CP Paul Chagonja na Rais wa TCCIA Mhandisi Peter Chisawillo wakisaini hati ya makubaliano ya ushirikiano. Waliosimama kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Daniel Machemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...