Tunayo furaha kuwakaribisha kwenye ufunguzi wa tawi la CHADEMA Ohio siku ya Jumamosi hii tarehe 26 October 2013 kuanzia saa kumi jioni.
Shughuli hii ya ufunguzi itafanyika katika ukumbi wa Best Western Hotel Columbus North 888 E Dublin Granville Road Columbus Ohio 43229.
Wana Chadema na Watanzania wote toka pande zote za USA bila kujali itikadi ya vyama mnakaribishwa. Vyakula vya kinyumbani na vinywaji vitakuwepo. DJ Roger kutoka Washington DC atatuburudisha kwa Muziki. Tafadhali mtaarifu na mwenzako.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na:
Mwenyekiti wa tawi: Salva Muhaya 614-657-3552
Katibu wa tawi: Helen Ongara 614-205-6867
Katibu mwenezi: Rehema Mwenda 614-254-1631
Mweka hazina: Amarido Mushi 330-412-9429
Asanteni sana,
Mungu Ibariki Tanzania



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...