Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Jubilee Bw. George Alande akizungumza na waandishi wa habari pamoja na mawakala wa bima wanaofanya kazi kwa kushirikiana na Jubilee wakati wa mkutano wa kutoa elimu kwa jamii kuhusu bima mbalimbali na faida zake iliyofuatiwa na hafla fupi ya kuwakabidhi zawadi baadhi ya wakala hao ikiwa ni sehemu ya shukrani na kutambua utendaji wao mzuri.
Meneja Rasiliamali watu kutoka Kampuni ya Bima ya Jubilee bi. Gloria Ngasa (kulia) akikabidhi zawadi ya laptop kwa mshindi wa tatu Bw. Kassa. A. Kassa ambaye ni mmojawapo wa mawakala wa bima wanaofanya kazi kwa kushirikiana na kampuni ya Jubilee nchini. Zawadi hiyo ni moawapo ya shukrani au kutambua utendaji mzuri wa mawakala hao.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya bima ya Jubilee Bw. George Alande (mwenye suti) akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi wa kampuni ya bima ya Venture Bw. Alex Lemnge (kulia) ambao pia ni washindi wa kwanza kati ya mawakala yanayofanya kazi kwa kushirikiana na kampuni ya bima ya Jubilee hafla hiyo fupi iliyoambatana na elimu ya bima kwa jamii ncini lifanyika jana katika hoteli ya New Africa Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...