TAWALA WA MIKOA
Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa kompyuta wa kusimamia rasilimali watu Serekalini, kwa Makatibu Tawala wa mikoa (RAS) na Wakurugenzi (DED) kutoka mikoa na wilaya mbalimbali Tanzania.
Maofisa hawa wa Serikali wamegawanywa katika makundi na watahudhuria mafunzo hayo kwa siku tatu tatu. Mafunzo hayo yanafanyika katika maabara za kompyuta za Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (Tanzania Global Learning Agency, TaGLA).
Katibu
Mkuu Bw. Yambesi (katikati) akifungua rasmi mafunzo hayo. Kushoto ni Bw. Mlay,
mkurugenzi rasilimali watu wizara ya utumishi, na kulia ni Bw. Senkondo,
mkurugenzi mkuu, TaGLa. Mafunzo haya yanafuatiwa na mafunzo mengine
yaliyotolewa kwa maafisa rasilimali watu wa mikoa, wilaya na taasisi zote za
UMMA Tanzania.
Dr.
Faisal, Katibu Tawala – Kilimanjaro, akisema neon kwa niaba ya washiriki wa
mafunzo.
Mafunzo haya yatawaweza maafisa hawa
kuufahamu mfumo wenyewe, kujua jinsi mfumo unavyofanya kazi na kufahamu jinsi ya kutumia taarifa zilizo
kwenye mfumo huu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka.
Washiriki
wa mafunzo
Makatibu
Tawala katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Kundi la kwanza la Wakurugenzi
katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Kundi la pili la Wakurugenzi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi








Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...