MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu,jijini Dar es Salaam, imeendelea kupiga kalenda kutoa uamuzi wa malalamiko ya ya kuwafutia kesi au la,  mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam,Abubakar Marijan [50] ‘Papaa Msoffe na Makongoro Joseph Nyerere kwasababu upande wa jamhuri kwa mara nyingine leo umewasilisha taarifa mpya ilieleza kuwa jarada hali la kesi hiyo limepelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwaajili ya Maelekezo zaidi.

Kesi hiyo ilipigwa kalenda jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa jalada bado linashikiliwa na Mwanasheria wa Kanda ya Dar es Salaam.

Hakimu Riwa alisema washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu hadi Novemba 14, mwaka huu kesi yao itakapotajwa. Hata hivyo, Makongoro hakufikishwa mahakamani hapo kusikiliza kesi yake kwa madai kwamba ni mgonjwa na hivyo Papaa Msofe alisikiliza kesi hiyo peke yake.

Papaa Msoffe ameshakaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa tangu alipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Agosti 12, mwaka 2012 akikabiliwa na shitaka la kumuua kwa kukusudia Onesphory Kituli, kinyume cha kifungu cha 196 cha Kanuni za Adhabu sura ya 19 kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka, 2002.

Ilidaiwa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo Oktoba 11, 2011, nyumbani kwake Kituli, Magomeni Mapipa, wilayani Kinondoni washtakiwa walitenda kosa hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...