MAHAKAMA ya Rufani Tanzania, jana imeshindwa kusikiliza rufaa ya kesi inayowakabili raia wawili wa China Hsu Chin Tai na Zhao Hanquing dhidi ya kufanya uvuvi haramu katika eneo la Kiuchumi la Bahari ya Hindi upande wa Tanzania baada ya mrufani wa kwanza kuomba kubadilisha wakili.

Hatua hiyo ilifikiwa jana baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Biswalo Mganga kuomba kesi hiyo kuahirishwa kutokana na mrufani wa pili Hanquing kuwasilisha hati ya kuomba kubadilishwa wakili.

Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa jana na jopo la majaji watatu likiongozwa na Mwenyekiti Jaji Salum Masati, akisaidiana na Jaji Bethuel Mmila na Semistodes Kaijage.

Hata hivyo, baada ya maombi hayo kutoka kwa mrufani huyo kuomba kumbadilisha wakili Amour Hamis na kusitisha kutetewa na wakili John Mapinduzi. Jaji Kaijage alisema kutokana na sababu hiyo mahakama inaahirisha kusikiliza rufaa hiyo hadi msajili wa mahakama hiyo atakapopanga tarehe nyingine ya kuisikiliza.

Mapema Mahakama Kuu ya Tanzania, iliwahukumu raia hao kwenda kulipa faini ya Sh. Bilioni 21 au kwenda jela miaka 10 baada ya kupatikana na hatia ya kuingia na kufanya shughuli za uvuvi katika eneo la kiuchumi la bahari ya Hindi.

Pia washtakiwa wanadaiwa  kuiingia eneo la bahari hiyo isivyo halali kinyume na sheria ya nchi. Hata hivyo, mahakama hiyo iliwaachia huru washtakiwa 34 kati yao waliokuwa wanakabiliwa na kesi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...