Pale familia zinapoamua kusonga mbele na maisha yanayohusisha watu zaidi ya waliokuwepo awali, mambo mengi hutokea. Kuna wakati ambao watoto huonekana kutokuwa tayari kupokea ujio wa watu wengine kwa kudhani watapoteza sehemu ya hadhi yao ndani ya nyumba (ama unaweza kusema wanakuwa na namna fulani ya wivu)
Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema akiwa na mgeni wake Mayor Mlima ndani ya studjio wakati wa kipindi.
Lakini pia, hata wazazi wanaoingia katika maisha ya familia nyingine hushindwa kurekebisha mwenendo wao kuweza kuwafaa watoto wanaowakuta na matokeo yake kuleta namna ya kutoelewana baina yao.
Tunaweza kuangalia sababu mbalimbali zinazosababisha haya, na kunaweza kuwa na sababu nyingi zaidi ya tunazoweza kufikiria juu ya hili, lakini tunaamini kuwa yapo mambo ambayo kama tutayazingatia, yanaweza kutupa mwanga wa kuepuka hili.
Georgina Lema akiendesha kipindi. Pembeni ni "fundi mitambo" wake Mubelwa Bandio
Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production kinachokujia kila Jumatatu, ambapo katika kipindi hiki, tumeanza na sehemu ya kwanza ya mfululizo wa vipindi vyetu vitakavyozungumzia changamoto za FAMILIA ZA KUFIKIA.
Yaani, kuwa mzazi wa kufikia, ama wengine wanasema MZAZI WA KAMBO.
Je! Ilikuwaje zamani? Ikoje sasa na kubwa zaidi tutajaribu kuangalia...Je! ilistahili kuwaje?
Katika kujadili hili, tumeungana na wazazi kujadili mada hii, na pia kusoma makala za uchunguzi juu ya hili.
Georgina Lema akijadiliana jambo na msimamizi wa kipindi chake Abou Shatry kuhakikisha kila kitu kiko sawa kabla ya kipindi.
Twawapenda...Tukutane juma lijalo katika muendelezo wa kipindi hiki kuhusu FAMILIA ZA KUFIKIA / FAMILIA ZA KAMBO
Karibu sana msikiliza hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...