Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza wakati akifungua mjadala wa vijana kuhusu dawa za kulevya, uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar.
Mratibu wa mradi wa JEE NIFANYEJE, kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Washington, Bi. Khadija Riyami, akizungumza kabla ya kumkaribisha Maalim Seif, kufungua mjadala wa vijana kuhusu dawa za kulevya, uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar. Mradi huo unajihusisha na maamuzi ya kiafya na kijamii kwa vijana.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na vijana wa “Sober houses’ baada ya kufungua mjadala wa vijana kuhusu dawa za kulevya, uliofanyika hoteli ya Bwawani Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kwa kuwatumia hao vijana vizuri(informer wenu-kwa kuwalipa pesa kama wafanyakazi wa kitengo cha kuzuia madawa ya kulevya)mtapata majina ya wote wanaojihusisha na uuzaji wa madawa.
    Lakini kama kuna viongozi ndio wahusika basi tutabaki tu kuwatibu na wengine kuharibika na hapatakuwa na suluhisho.
    Ni maoni yangu tu...

    ReplyDelete
  2. Hawa vijana waajiriwe kwenye kitengo cha madawa ya kulevya ili walete majina ya wanaoingiza nchini madawa(sembe).
    Mtakuwa mmewasaidia sana kuinua maisha yao na wao watakuwa wanawasaidia sana kuondoa hili balaa kwenye nchi yetu.
    Vinginevyo tutatwanga maji kwenye kinu tu.....

    ReplyDelete
  3. Nakuona Twahir a.k.a. "Jibaba" na baadhi ya wana "Sober Houses" ulioambatana nao. Nazidi kuwaombea kila la kheri. IN SHA ALLAH, Mwenyeez Mungu atazidi kuwaongoa na kuwaelekeza palipo pema na penye kheri zake, awanusurishe na shari, vishawishi pamoja na mabaya yote katika ulimwengu huu - AMEEN.

    Kwa kweli Inatia moyo sana kwa kuona mmeweza kujitambuwa na kuzielewa athari zake.

    ReplyDelete
  4. Waachane na miktadha ya triggers za kulevya; la sivyo, kazi bure!
    Once addict, always addict!

    ReplyDelete
  5. Mdau shauri la kuwatumia hao kuwataja na kuwakamata wanaoingiza madawa ya kulevya limeshasemwa mara nyingi, tatizo sio kama hawajulikani ila ni wakubwa, ni jamaa wa wakubwa au wana link na serikali ikiwa pamoja na kufadhili chama tawala, kama unatoka zanzibara ua unaishi zanzibar utajua nawakusudia akin nani kwani sote zanzibar tunawajua vyema tu

    ReplyDelete
  6. mdau uliesema once addict, you are an idiot and once an idiot is always and idiot

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...