Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo Amefurahishwa na kasi ya utandazaji na uunganishwaji wa mabomba ya gesi unaoendelea nchini ili kuwezesha kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam na kutumika katika uzalishaji wa umeme katika mitambo ya kufulia umeme itakayojegwa Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Muhongo, amewataka watanzania kuwapuuza wale wote wanaobeza mradi wa ujenzi wa bomba hilo la gesi na kwamba hakuna haja ya kuwasikiliza kwa imani kuwa hawajui umuhimu wa mradi huu katika kukuza uchumi wa watanzania.
Muhongo ameyasema hayo wilayani Mkuranga wakati wa ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba katika uunganishwaji wa mabomba hayo yanayotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2014.
Ameeleza kuwa ujenzi wa mabomba ya gesi unaendelea vizuri na kwamba kuna vikosi vitano ambapo wengine wanajenga kuanzia Mtwara kuelekea Dar es Salaam na wengine wanaanzia Dar es Salaam kwenda Mtwara ili kukamilisha kilomita 542 za mradi wote.
Balozi wa China nchini Bw. Lu Youqing, ameuhakikishia umma wa watanzania kwamba ujenzi wa bomba unaoendelea umejegwa kwa technolojia ya hali ya juu na kwa umakini mkubwa ambapo viwango vyake viko juu zaidi ya vile vya kimataifa.
Baloziamesisitiza uwepo wa uhuru, Urafiki na Demokrasia katika kutimiza azma ya kukamilisha ujenzi huo ambapo ametamka wazi kuwa kuna uwezekano mkubwa wa mradi kuisha kabla ya wakati uliopangwa kutokana na kasi na juhudi waliyonayo wafanyakazi katika ujenzi huo.
Muhongo ameelezwa kuwa mabomba yaliyolazwa na yanayofanyiwa kazi yanakamilisha kilomita 104 ambapo tayari km 34 zimekwishaunganishwa kwa kuchomelewa ikiwa ni hatua ya awali ambapo km 6 zimesilibwa ili kuzuia nafasi ya gesi kuweza kupenya na kupotea. Hayo yameelezwa na mhandisi wa bomba la gesi toka shirika la Maendeleo ya Mafuta nchini (TPDC) injinia Baltazari Thomas.
Akielezea changamoto zinazowakabili katika ujenzi wa bomba la gesi, Peter Erasmus Manager wa mradi (QA/QG) amesema hali ya kunyesha mvua inakwamisha ujenzi wa mradi huo kwani ni vigumu na gharama kubwa kujenga kipindi hicho pia ni hatari kwa afya za wafanyakazi.
Hii ni mara ya pili kwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na Balozi wa China Ndg Lu Youqing kufanya ziara maeneo ambayo ujenzi wa mabomba unaendelea na kwamba wamekubaliana kutembelea maeneo hayo kila mwezi ili kuwapa hamasa wajenzi kuwa na kasi inayotakiwa na hivyo kuwezesha mradi kukamilika kwa wakati.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongozana na Balozi wa China nchini Bw. Lu Youqing wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa ujenzi wa mabomba ya gesi unaoendelea nchini ili kuwezesha kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam,unaoendelea katika wilaya ya Mkuranga.
Waziri wa Nishati na Madini akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika ofisi za mradi wa ujenzi wa bomba la gesi wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki nyuma yake ni balozi wa China nchini Dr. Lu Youquing
Profesa Sospeter Muhongo akipewa maelezo ya namna ujenzi unavyoendelea akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa bomba la gesi toka mtwara kuja Dar Es Salaam wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki.
Profesa Sospeter Muhongo akioneshwa kipande cha bomba kilivyosilibwa kwa utaalamu mkubwa ili kuziba mianya ya kuweza kupitisha gesi nje na hivyo kusababisha upotevu wa gesi kulia kwake ni balozi wa China nchini Tannzania.
Profesa Sospeter Muhongo akipewa maelezo ya namna ujenzi unavyoendelea akiwa katika ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa mradi wa bomba la gesi toka mtwara kuja Dar Es Salaam wilayani Mkuranga mwishoni mwa wiki.
Profesa Sospeter Muhongo akioneshwa kipande cha bomba kilivyosilibwa kwa utaalamu mkubwa ili kuziba mianya ya kuweza kupitisha gesi nje na hivyo kusababisha upotevu wa gesi kulia kwake ni balozi wa China nchini Tannzania.
MUNGUibariki Tanzania.
ReplyDeleteLabda kwa njia hii tutatokomeza umasikini.
MUNGU tuondolee ubinafsi wa wale wanaopewa majukumu.
Amina