Wajumbe wa Mkutano wa 23 wa wanachama na wadau wa Mfuko wa pensheni wa PPF, waliokuwa wakishiriki mkutano huo kwa siku tatu mfululizo,jana walipata fursa ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya Utalii wa ndani ili kuweza kujionyea vivutio mbali mbali ndani ya hifadhi hiyo iliopo ndani ya Mkoa wa Manyara.Pichani ni lango kuu la kuingia kwenye Hifadhi hiyo.

Baadhi ya Wakurugenzi wa PPF wakichukua taswira mbali mbali kupitia iPad's zao pindi waonapo wanyama kwenye hifadhi hiyo.
Mzee wa Nyika (kushoto) akionyesha tabasamu lake kwa Wadau wa PPF waliotembelea hifadhi hiyo ya Ngorongoro.
Waheshimiwa Wabunge,Mh. Titus Kamani na Mh. Amina Mwidau wakichukua taswiza za Wanyama mbali mbali ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro,wakati walipotembelea pamoja ya Wajumbe wa Mkutano wa 23 wa PPF.
Kiukweli Hifadhi hii inavutia sana  na inawanyama wengi sana.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa pensheni wa PPF, William Erio (Katikati mwenye fulana nyeupe), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi ya wadhamini ya mfuko huo, wakurugenzi wa idara na maafisa wengine baada ya kuona viboko walio kwenye bwawa la Makati.Picha zote na Othman Michuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...