Mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoa wa Pwani Mkurugenzi Rasilimali watu wa Dawasa Bi.Mary Ngonyani,akimkabidhi Cheti Anna Kiwali aliefanya vizuri katika masomo ya Hesabati na Sayansi wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Nne katika Shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Wanaoshuhudia, Kulia ni Mkurugenzi wa Shule hiyo Dr.Aumsuri Kiwelu na Mkuu wa shule hiyo Mtanga Gerson..JPG)
Baadhi ya wanafunzi kati ya 45 wanaosoma kidato cha Nne katika shule ya sekondari ya wasichana ya Luther iliyopo Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakimkabidhi zawadi ya kumshukuru mwalimu wao Mkuu Mtanga Gerson wakati wa Mahafali yao ya kwanza ya Kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 wanategemea kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha Nne hivi karibuni.Wapili kutoka kushoto ni Mkurugenzi Rasmali Watu Mary Ngonyani,ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo na Mkurugenzi wa shule hiyo Aumsuri Kiwelu.
Mtaalamu wa kutengeneza maabara za shule ,(Lab Technical) na mwalimu wa masomo ya Chemistry, Biology katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Luther iliyopo eneo la Mapinga Bagamoyo Mkoa wa Pwani Bw.Kalistus Mwendapole akimuonesha Mkurugenzi Rasmali Watu Mary Ngonyani,alipotembelea maabara ya shule hiyo akiwa mgeni rasmi wa mahafali ya kwanza ya kidato cha Nne tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2010. Jumla ya wanafunzi 45 wanategemea kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha Nne hivi karibuni.
nilitegemea hiyo demostration ingefanywa na mwanafunzi instead of Teacher,ingeleta maana zaidi
ReplyDeleteHongera Luther Sec School kwa mahafali ya kwanza ya kidato cha 4; Kwa upande mwingine ingekuwa vizuri sana kama picha hizo za hapo maabara zingeonyesha wanafunzi wakifanya experiment na siyo lab Technician au Mwalimu wa shule hiyo.....ikiwa mmewafundisha watoto na sasa wana-graduate basi habari hii ingeenda sambamba na kazi za maabara zinazofanywa na wanafunzi na siyo waalimu/Lab Technicians (ni mtazamo tu!)
ReplyDelete