WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewahimiza viongozi wa Kanisa la Morovian Jimbo la Ziwa Tanganyika kuwekeza zaidi kwa vijana ambao ndiyo nguvukazi ya Taifa.
Ametoa wito huo leo mchana (Jumapili, Oktoba 6, 2013) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa mji wa Kigoma waliohudhuria Sherehe za Uzinduzi wa Jimbo la Ziwa Tanganyika Kanisa la Moravian Kigoma.
Waziri Mkuu ammbaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, alimuomba Askofu Dkt. Isack Nicodemo wa Kanisa la Moravian Tabora ambaye ndiye mlezi wa jimbo hilo jipya, kuhakikisha kuwa anawapeleka vijana wengi wa Kanisa hilo kwenye Chuo cha Kilimo cha Mubondo kilichopo wilayani Kasulu, Kigoma ambacho kinatoa mafunzo ya kilimo kwa vijana katika ngazi za Astashahada na Stashahada ya Kilimo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...