Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi TAnzania (TAMSA) lililofanyika jijini Mwanza leo, Oktoba 6, 2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Cheti kutoka kwa Mratibu wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi TAnzania (TAMSA) ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Hubat Kairuki cha Dar es Salaam, Helga Mutasingwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Mhe. Makamu katika kufanikisha Kongamano hilo. Makamu alipokea Cheti hicho leo Oktoba 6, 2013 baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Afya, Dkt. Hussein Mwinyi (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Evarist Ndikilo, wakijumuika kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...