Maonyesho makubwa ya sekta ya nyumba yajulikanayo kama Tanzania Homes Expo yamefunguliwa rasmi leo na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Prof. Mbarawa. Akiongea baada ya kutembelea mabanda mbali mbali alisema 
‘’ Inafurahisha kuona watoa huduma mbalimbali binafsi na wa serikali wako hapa kutoa taarifa na kuonyesha masuluhisho mbali mbali ya ujenzi. Napenda kuchagiza umuhimu wa kutumia Tehama katika kuboresha maisha ya wakazi’’. 
Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group ambao ni waandaaji na wamiliki wa Tanzania Homes Expo alisema ‘’ Ukuaji wa idadi ya watu na upatikanaji wa makazi havina uwiano sawa, hii ni changamoto ambayo inaweza kutatuliwa kwa kuwawezesha wananchi kuwa na makazi hivyo maonyesho ya Tanzania Homes Expo yanawawezesha wananchi kukutana na kufahamu huduma au kupata ushauri wa sekta pana ya makazi’’. 
Maonyesho ya Tanzania Homes yamedhaminiwa na CAM Gas, Camel Cement, African Life, CRDB na NHIF.Maonyesho hayo yameanza tarehe 14 na yataisha tarehe 15.
Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Prof. Mbarawa akifungua maonyesho ya Tanzania Homes Expo. Kushoto ni Imani Kajula Mkurugenzi Mtendaji wa EAG Group, Kulia ni Oscar Mgaya Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC. Wengine ni viongozi wa Camel Cement and CAM Gas.
Sehemu ya umati wa watu wakitembelea watoa huduma za sekta ya nyumba.
NHC ambao ni kati ya wadau wakubwa wa sekta ya nyumba nao wapo.
Umati wa watu waliofika kutembelea maonyesho ya Tanzania Homes Expo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Imani lazima MCHAWI, inakuaje kila unachoshika kinakuwa Almasi? Huyo mganga lazima unionyeshe nikirudi Tanzania.

    ReplyDelete
  2. maonyesho yako wapi?

    ReplyDelete
  3. katika kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa lazima Watanzania tuwe na uthubutu wa kutekeleza yale yote Mwalimu aliyotuasa na kutuachia. Mfano Mwalimu alichukia sana mambo ya Ufisadi, Udini, Ukabila, Unyonyaji, uroho wa madaraka sasa hivi hali imekuwa sivyo kabisa. Watanzania, Viongozi tumuenzi Mwl. Baba wa Taifa kwa vitendo jamani!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...