Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Amos Makala akizungumza na wakazi wa manispaa ya Iringa wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Kajugusi akitoa ufafanuzi kuhusu Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kila mwaka nchini wakati wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma wakiangalia banda la Maonyesho la vijana wajasiriamali kutoka Zanzibar wanaoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiangalia gari lililotengenezwa kwa kutumia mbao na vifaa vya asili na mbunifu Keny Joseph kutoka kijiji cha Nyororo, Mufindi. Gari hilo ambalo limekua kivutio kikubwa katika maonyesho hayo analitumia katika shughuli zake za kila siku na lina uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 180 kwa saa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiingia ndani ya gari hilo.
Hilo gari lingetafutiwa jina la asili hivi, badala ya kuliandika toyota
ReplyDeleteHakika mdau hapo juu umeshauri jambo Jema. Bado baadhi yetu watz tunashobokeaga majina ya wadhungu. Tuache! Lingeitwa ''Mabua''
ReplyDeletelinatakiwa liwe na fire extinguisher sita kwa uchache au kila linakokwenda gari la fire liwe nyuma yake.
ReplyDelete