Naibu Waziri wa Habari, Vijana ,Utamaduni na Michezo Amos Makala akizungumza na wakazi wa manispaa ya Iringa wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Bw. James Kajugusi.
Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Kajugusi akitoa ufafanuzi kuhusu Maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kila mwaka nchini wakati wa Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na kuwataka vijana kutumia fursa za kiuchumi zilizopo kujiletea maendeleo.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiwa ameambatana na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma wakiangalia banda la Maonyesho la vijana wajasiriamali kutoka Zanzibar wanaoshiriki Maonyesho ya Wiki ya Vijana mkoani Iringa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiangalia gari lililotengenezwa kwa kutumia mbao na vifaa vya asili na mbunifu Keny Joseph kutoka kijiji cha Nyororo, Mufindi. Gari hilo ambalo limekua kivutio kikubwa katika maonyesho hayo analitumia katika shughuli zake za kila siku na lina uwezo wa kusafiri umbali wa kilometa 180 kwa saa.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amosi Makala akiingia ndani ya gari hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hilo gari lingetafutiwa jina la asili hivi, badala ya kuliandika toyota

    ReplyDelete
  2. Hakika mdau hapo juu umeshauri jambo Jema. Bado baadhi yetu watz tunashobokeaga majina ya wadhungu. Tuache! Lingeitwa ''Mabua''

    ReplyDelete
  3. linatakiwa liwe na fire extinguisher sita kwa uchache au kila linakokwenda gari la fire liwe nyuma yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...