
Mimi ni Ndugu Mtenga kutoka Tanzania na kwa sasa nafanya kazi Portland Oregon USA.
Langu ni ombi la habari kuhusu msichana wa miaka 8 aliyeogelea na kitoto kichanga mgongoni kutoka kwenye ajali ya mashua( Boat) iliyozama ziwani Tanganyika.
Naomba kama una hiyo habari utakuwa umenisaidia sana maana nataka kutafuta njia yakumzawadisha huyo mtoto.
Email yangu ni kama itakavyojitokeza bali pia nivizuri nikaiandika hapa djmtenga@yahoo.com.
Nawatakia kila la heri nikiwa
na matumaini kwamba nitapata msaada ninaotarajia.
Mdau Mtenga


Nakuunga mkono kwa wazo lako be blessed ni watu wachache mliobaki nimevutiwa na habari ile...nashukuru kuona Mungu amekupa ujasiri huo
ReplyDeleteMCHAGGA WA KWELI WEWE, HONGERA SANA KWA UJARI WAKO.
ReplyDeletekwa kweli sikuiona hiyo habari ila napenda kuunga mkono na pia akipatikana naomba awekwe hapa hata sisi tumpe pongezi na ushujaa huo. pia bila shaka at age of 8 kuogelea hivyo inaweza kuwa ni kipaji kikubwa sana.. hongera mdau kwa wazo zuri sana ..Naunga mkono hoja.
ReplyDeleteMimi Pia sijaona Habari hiyo, Naomba Akipatikana huyo mtoto anuani zake zipatikane tufanye linaloo wezekana, Ameokoa maisha ya watu wengi sana hapo, Ukiangalia kwa haraka haraka utaona ni maisha ya watu wawili tu but ni zaidi ya wawili,pia huyo mtoto ni Commando. Anatakiwa endelezwa. mtumzima tu unapagawa ikitoa jambo kama holi sasa mtoto tena chini ya miaka kumi anakuwa jasiri kwa kiasi hicho hiyo sio kawaida. Habari zake zinatakiwa sikika sana. Nakama inawezekana achangiwe kama yule alie okota mkoba mareklani akachangiwa mamilioni hata sisi tunaweza,ile page ipo na ya bure tu, tutaanzisha campaign kule ya kuchangiwa.
ReplyDelete