Mikutano ya mwaka ya Bodi ya Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia kwa mwaka 2013 imeanza rasmi leo mjini Washington D.C. Mikutano hii itafikia kilele chake hapo tarehe 11 – 13, mwezi Octoba ,2013.
Bodi ya Magavana wa kundi la Benki ya Dunia ( Benki ) na Bodi ya Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa ( Mfuko) kwa kawaida hukutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi za Taasisi zinazowahusu. Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi mwanachama.
Waziri wa Fedha wa Tanzania Mhe. Dkt. Willium Mgimwa , Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dr. Silvanus Lekwilile pamoja na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu wao ni Magavana wa mikutano hiyo. Nchi karibu zote zimeshawasili katika mikutano hii.
‘Lengo la mikutano hii kwa nchi ya Tanzania, inatupa nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za mapato na matumizi.
"Nia yao kubwa ni kutusaidia na kusikia tuna mawazo gani na maeneo gani wanaweza wakatusaidia katika kuboresha na kuangalia kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri’. amesema Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa alipokuwa akijadiliana na ujumbe kutoka Tanzania.
Aidha Mhe. Dkt. Mgimwa alisema kuwa, Katika mazungumzo na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la Kimataifa, ujumbe wa Tanzania utawasilisha hali halisi ya utendaji wa kiuchumi wa Tanzania na hali ya matumizi na mapato ya fedha na mambo yanayohusiana na taasisi zinazoendesha nishati kama vile Shirika la umeme Tanazania (Tanesco) na shirika la maendeleo ya mafuta Tanzania (TPDC) pamoja na kutazama mienendo ya madeni yetu na mwenendo wa mapato kwa ujumla.
Hali ya hewa mjini hapa ni ya manyunyu na mvua za hapa na pale.
Imetolewa na:
Ingiahedi Mduma
Msemaji Mkuu
Wizara ya Fedha
Washington D.C
7/10/2013
Kutoka kulia ni Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Dr. Philip Mpango, Naibu Gavana wa BOT Bi. Natu Mwamba na Mchumi wa Benki Kuu Bi. Sauda Msemo wakisikiliza kwa makini.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa (kushoto), Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Silvacius Likwelile akitoa ufafanuzi.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Wiliam Mgimwa akiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania kuhusu maandalizi ya mikutano na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...