Profesa Ali Mazrui akizungumza wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere ambayo hufanyika kila Octoba 14, kwa mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza katika Umoja wa Mataifa na kuhudhuriwa na mabalozi wa mataifa mbambali pamoja na watanzania waishio jijini New York na vitongoji vyake. Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Elliasson kwa niaba ya Katibu Mkuu, Profesa alimuuelezea Mwalimu Nyerere kama kiongozi ambaye ameawachia watanzania na dunia uridhi wa aina yake na hasa urithi wa muungano ambao anasema licha ya changamoto zake bado unaendelea kudumu na kuwa mfano wa kuigwa barani afrika na duniani kote.
Profesa Ali Mazrui akiwa ameshika kitabu alichokiandika kwa kushurikiana Profesa Lindah Mhando, kitabu hicho kuhusu Mwaliumu Julius Kambarage Nyerere kilizinduliwa rasmi wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere Day ambayo hufanyika Octoba 14. Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ambayo kwa mara ya kwanza yalifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwa kuratibiwa na Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Profesa Ali Mazrui anasema alimfahamu Mwalimu kwa zaidi ya miaka 40, walishirikiana katika mijadala ya kisiasa, walitaniana lakini waliheshimiana pia. Anasema daima hata sahau muda na nyakati alizokuwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Profesa Ali Mazrui unahitajika kuja kutoa somo SUZA (State Univesrity of Zanzibar) !!!
ReplyDeletewaambie wenzio prof.
ReplyDeletehaswa wanao na wajukuu zako kwa rika maana huko ndiko shida ilipo
SALAMU KWA WAPINGA MUUNGANO:
ReplyDeleteMmeona eee?
Profesa wa nchi Jirani Jamhuri ya Kenya anaona umuhimu wa Muungano huku wapinga muungano mkwa weupeee kiakili!!!
Hivi Wapinga Muungano Visiwani mnakwenda na wakati tuliokuwa nao?
Dunia nzima kila sehemu inatafuta Muungano wakati ninyi mnapinga Muungano !!!
Mdau wa Kwanza:
ReplyDeleteHio Lecture ya Prof. Ali Mazrui hapo SUZA (State University of Zanzibar) itabidi aitoe chini ya Ulinzi mkali wa Polisi,,,!
Tusije shangaa wana Uamsho wakakerwa na Lecture na wakamwagia usoni Prof. Mazrui Tindikali!
Michizi tunaweza kukipata wapi hiko kitabu sisi watu wa ughaibuni ...plzzz.
ReplyDeletemdau wa Ukerewe