Wakazi wa Kijiji cha Ndungu Wilayani Same,wakiangalia Greda likiendelea na kazi ya kusawazisha njia mara baada ya kumomonyoka kwa udongo katika eneo linalojengwa Daraja na kupelekea magari kushindwa kupita kwa muda.hali hiyo imekuja kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha Wilayani humo.zoezi hili lilichukua takribani saa moja na nusu na kufanikiwa kupita kwa magari yaliyokuwa yamekwama kupisha zoezi hilo.
Sehemu iliyomomonjoka kutokana na wingi wa maji ya mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.
Kazi ikiendelea.
Baadhi ya magari na pikipiki yakiwa yamesimama kupisha zoezi la usawazishaji wa njia.
Magari yalianza kupita japo ilikuwa ni kwa shida.
Alafu hii barabara si imekabidhiwa juzijuzi tu kwa sherehe na nderemo.....lahaula ama kweli......
ReplyDelete